· Kila
mwajiri anapaswa kuijuilisha Bodi mtumishi mpya anayeajiriwa ndani ya miezi
mitatu ili Bodi ijiridhishe kama mwajiriwa huyo ni mdaiwa wa Bodi au la.
· Ikithibitika
kuwa mwajiriwa ni mdaiwa wa Bodi, mwajiri atapaswa kukata kiwango cha deni
kutoka kwenye mshahara wa kila mwezi wa mdaiwa kwa utaratibu ambao Bodi itaona
unafaa.
· Mwajiri
atawajibika kuwasilisha mikato ya mshahara wa kila mwezi wa mdaiwa si zaidi ya
siku 15 za mwezi unaofuata kwa utaratibu utakaotolewa na Bodi.
· Kwa kukubali kumwajiri mdaiwa wa BMEJZ, mwajiri hatokuwa na nafasi ya kukwepa wajibu wake wa kuanza kukata mshahara wa mdaiwa na kuwasilisha marejesho kwa BMEJZ kwa kisingizio cha kutokuwa mshiriki katika mkataba wa mkopo kati ya BMEJZ na mdaiwa.
Adhabu kwa Mwajiri Anayekiuka
Wajibu Wake
Mwajiri atakayeshindwa kutekeleza wajibu
wake ipasavyo anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria zifuatavyo:
·
Kutozwa faini au tozo nyengine yoyote ile
ambayo Bodi itaona inafaa kwa kuchelewa kuwasilisha kwa wakati mikato ya
mshahara wa mdaiwa kwenye ofisi za Bodi (Kifungu cha 27(1) cha Sheria ya Bodi).
·
Kutozwa faini inayofikia shilingi milioni tano
au kufungwa jela kwa kifungo kisichopungua miezi 12 au adhabu zote mbili kwa
pamoja kwa kushindwa kukata deni la mdaiwa wa Bodi kutoka kwenye mshahara wake
na kuwasilisha mikato hiyo kwenye ofisi za Bodi (Kifungu cha 27(2) cha Sheria ya
Bodi).
·
Kulipa deni lote linalodaiwa pamoja na tozo
nyenginezo ambazo Bodi itaona zinastahiki kulipwa (Kifungu cha 27(3) cha Sheria ya
Bodi).