News

WALIOTEULIWA KUPATA MIKOPO 2020/2021 - PHD

2020-12-05 09:02:59.0 Download

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR (BMEJZ) INAWAJULISHA WAOMBAJI WOTE WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU  KWA MWAKA WA MASOMO 2020/21 KUWA IMEKAMILISHA UTEUZI WA AWAMU YA KWANZA.

MAJINA YA WAOMBAJI WALIOTEULIWA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI ZA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (www.zhelb.go.tz) NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI (www.moez.go.tz).

WAOMBAJI WOTE WALIOTEULIWA KUPATA MKOPO WANATAKIWA KUZINGATIA YAFUATAYO:

 

·        KILA MUOMBAJI ALIYETEULIWA ATALAZIMIKA KUJAZA MKATABA WA MKOPO AMBAO UTAJAZWA KWA KUTUMIA MFUMO WA ‘’ZOLAS’’ UNAOPATIKANA KATIKA AKAUNTI BINAFSI ZA WAOMBAJI WA MIKOPO. HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAYEFANYIWA MALIPO YOYOTE BILA YA KUJAZA NA KUTUMA MKATABA.

·        KILA MWANAFUNZI ALIYETEULIWA ANAPASWA KULIPA ADA YA MIKATABA YA TZS 35,000 KUPITIA MIFUMO YA MALIPO YA SIMU ZA MKONONI BAADA YA KUPATIWA NAMBARI YA KUMBUKUMBU (REFERENCE NUMBER) YA MALIPO KWENYE AKAUNTI YAKE YA ZOLAS.

·        WAOMBAJI WOTE WALITEULIWA KUPATA MIKOPO KUTOKA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TANZANIA (HESLB) WANATAKIWA KUENDELEA NA MIKOPO HIYO.

·        MIKOPO INAYOTOLEWA NA BMEJZ KWA WAOMBAJI WAPYA WA MWAKA WA MASOMO 2020/21 HAIWAHUSU WAAJIRIWA WA SMZ NA SMT KAMA ILIVYOARIFIWA WAKATI WA KUTUMA MAOMBI.

·        MUDA WA MWISHO WA KUJAZA MIKATABA KWA WANAFUNZI WAPYA NI TAREHE 13 DISEMBA, 2020.

TANBIHI:

KWA UFAFANUZI WA SUALA LOLOTE LINALOHUSU MIKOPO PAMOJA NA NAMNA YA KUENDELEA NA UJAZAJI WA MIKATABA YA MIKOPO KWA KUTUMIA MTANDAO WASILIANA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR KWA KUFIKA MOJA KWA MOJA KATIKA OFISI ZAO ZILIZOPO KATIKA JENGO LA SINEMA YA MAJESTIC VUGA ZANZIBAR NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI CHAKECHAKE PEMBA AU KWA KUTUMIA NAMBARI ZIFUATAZO:

ZANTEL - 0777 348967 AU 0777 348973 ,

e mail: info@zhelb.go.tz

 

LIPA MKOPO NA WENGINE WASOME