Nafasi za ufadhili wa masomo
Kuanzia mwaka wa masomo 2016/17, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia BMEJZ imeanzisha utaratibu wa kutoa nafasi za ufadhili wa masomo (scholarships) kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika mitihani ya Taifa ya kidato cha sita. Walengwa wa ufadhili wa masomo watakuwa wanafunzi wa kidato cha sita wa masomo ya sayansi wenye ufaulu mzuri zaidi katika mitihani yao ya taifa ya kidato cha sita. Kila mwaka kutatolewa nafasi kumi (10) kwa...