mersin escort porn

 

T A N G A Z O

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu - Zanzibar inatangaza nafasi za masomo kwa ngazi ya shahada kwanza katika fani za sayansi tu kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kupitia Shirika la Benki ya Kiislamu (IDB).

Sifa za Muombaji

  • Awe Mzanzibari.
  • Awe amemaliza masomo ya Kidato cha Sita na kufaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili.
  • Awe na umri usiozidi miaka 24 ifikapo Julai 2020.
  • Asiwe mwanafunzi anaendelea na chuo chochote.

Taratibu za Maombi

Waombaji wote wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mtandao ufuatao https://isdbscholarship.smartsimple.com. Ukiambatanisha na vyeti vya mitihani ya Taifa na cheti cha kuzaliwa.

Aidha kuwasilisha vivuli vya maombi hayo katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar jengo la Majestik sinema kwa Unguja na jengo la Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Chakechake Pemba.

Maombi yanapatikana katika mtandao wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (www.zhelb.go.tz)

Mwisho wa kutuma maombi hayo ni tarehe 28 Februari, 2020.