mersin escort porn

zhelb


BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR (BMEJZ) INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA IMEKAMILISHA UTEUZI WA AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WATAKAOPATIWA MIKOPO YA ELIMU YA JUU NA NAFASI ZA UFADHILI WA WASOMO WA SMZ KWA MWAKA WA MASOMO 2019/20 KWA VYUO VYA NDANI NA NJE YA NCHI.

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOTEULIWA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR (www.zhelb.go.tz) NA TOVUTI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR (www.moez.go.tz).

WANAFUNZI WALIOTEULIWA WANATAKIWA KUFIKA KATIKA OFISI ZA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR ZILIZOPO KATIKA JENGO LA MAJESTIC CINEMA VUGA KWA WALIOPO UNGUJA NA JENGO LA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI CHAKE CHAKE KWA WALIOPO PEMBA KUANZIA TAREHE 28/10/2019.

INASISITIZWA KILA MWANAFUNZI ALIYETEULIWA ANAPASWA KUJAZA MKATABA MAALUM WA MKOPO UNAOTOLEWA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR KABLA YA KUANZA KUPATIWA MKOPO HUO.

WANAFUNZI WALIOTEULIWA WANATAKIWA KUCHUKUA KITAMBULISHO CHA MZANZIBARI NA “BANK PAY IN SLIP” KUTHIBITISHA KUFANYA MALIPO YA TZS 35,000 KATIKA AKAUNI Na. 0406017000 YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR ILIYOPO KATIKA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ) KWA WALIOPO UNGUJA. KWAWALIOPO PEMBA MALIPO YAFANYWE KWENYE AKAUNTI Na. 0712760001 YA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR ILIYOPO KATIKA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR (PBZ) KWA WALIOPO UNGUJA.

INDHARI

WANAFUNZI WALIOPATA MIKOPO KUTOKA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU YA SERIKALI YA MUUNGANO (HESLB), MAJINA YAO YATAONDOSHWA KATIKA UTEUZI WA WANAFUNZI WATAKAOPATIWA MIKOPO INAYOTOLEWA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR ILI KUHAKIKISHA KUWA HAKUNA MWANAFUNZI ANAYEPATA MIKOPO KUTOKA BODI ZOTE MBILI KAMA SHERIA INAVYOELEKEZA.

KWA WANAFUNZI WALIOPATIWA MIKOPO NA HESLB NA BMEJZ NA WANATAKA KUENDELEA NA MIKOPO YA BMEJZ WANATAKIWA KUANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI WA BMEJZ NA KUAMBATISHA UTHIBITISHO WA KUTOENDELEA NA MIKOPO YA HESLB.

AWAMU YA TATU YA UTEUZI WA MAJINA YA WANAFUNZI WATAKAOPATIWA MIKOPO INAENDELEA KUSHUGHULIKIWA NA MAJINA YATATANGAZWA BAADAYE