News

MAELEKEZO KWA WATEULIWA WA MIKOPO

2021-10-23 11:32:10.0

WAOMBAJI WOTE WALIOTEULIWA KUPATA MKOPO PAMOJA NA UFADHILI WA SMZ WANATAKIWA KUZINGATIA YAFUATAYO

1.    KILA MWOMBAJI ALIYETEULIWA ATALAZIMIKA KUJAZA MKATABA AMBAO UTAJAZWA KWA KUTUMIA MFUMO WA ‘’ZOLAS’’ UNAOPATIKANA KATIKA AKAUNTI ZA WAOMBAJI WA MIKOPO. HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAYEFANYIWA MALIPO YA GHARAMA ZA MASOMO BILA YA KUJAZA MKATABA WA MKOPO.

 

2.    MWOMBAJI ALIYEPATA MKOPO KUTOKA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TANZANIA (HESLB) ATAFUTWA KATIKA ORODHA YA WAOMBAJI WALIOPATIWA MIKOPO NA BMEJZ ILI KUEPUSHA MWOMBAJI MMOJA KUPATA MIKOPO KUTOKA BODI ZOTE MBILI KWA WAKATI MMOJA KINYUME NA SHERIA.

 

3.    MIKOPO INAYOTOLEWA NA BMEJZ KWA WAOMBAJI WAPYA WA MWAKA WA MASOMO 2021/22 HAIWAHUSU WAAJIRIWA WA TAASISI ZA UMMA ZA SMZ NA SMT. MWOMBAJI AMBAYE NI MWAJIRIWA NA JINA LAKE LIMEJITOKEZA KATIKA MAJINA YALIYOTANGAZWA ANAOMBWA ASIJAZE MKATABA NA BODI HAITOHUSIKA NA MADAI YOYOTE YA GHARAMA ZA MASOMO KATIKA CHUO ALICHOPATA UDAHILI.

4.    MUDA WA MWISHO WA KUJAZA MKATABA HUO WA MKOPO NI TAREHE 30 NOVEMBA, 2021.

5.    MAJINA YA WAOMBAJI WALIOTEULIWA YATAANZA KUTUMWA KATIKA VYUO HUSIKA KUANZIA TAREHE 25/10/2021

 

TANBIHI:

KWA UFAFANUZI WA SUALA LOLOTE LINALOHUSU MIKOPO PAMOJA NA NAMNA YA KUENDELEA NA UJAZAJI WA MIKATABA YA MIKOPO KWA KUTUMIA MTANDAO WASILIANA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR KWA KUFIKA MOJA KWA MOJA KATIKA OFISI ZAO ZILIZOPO KATIKA JENGO LA SINEMA YA MAJESTIKI VUGA ZANZIBAR NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI CHAKECHAKE PEMBA AU PIGA SIMU KWA KUTUMIA NAMBARI MAALUM ZIFUATAZO:

 

0777 348967 AU 0777348973

IMETOLEWA NA BODI YA MIKOPO ELIMU YA JUU ZANZIBAR